Simba SC imetinga hatua ya makundi kwa kuwaondoa Nsingizini Hotspurs kwenye CAF Champions League huku Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC akibainisha kuwa ambacho walikuwa wanahitaji ni kufuzu hatua ya makundi.
Oktoba 26,2025 wababe hawa wawili milango ilikuwa migumu katika dakika 90. Hivyo faida ya ushindi wa ugenini imewapa tiketi Simba SC kutinga hatua ya makundi kimataifa.
Kwenye mchezo wa kwanza ugenini ilikuwa Nsingizini Hotspurs 0- 3 Simba SC, Oktoba 19,2025. Ligi ya Mabingwa Afrika. Mabao ya Simba SC yalifungwa na Wilson Nangu na Kibu Dennis alifunga jumla ya magoli mawili kwenye mchezo huo.
Ahmed amesema: “Tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye burudani Uwanja wa Mkapa na wamelipa viingilio hili tunajivunia. Kushindwa kufunga haikuwa kwenye malengo makubwa ila muhimu ni kutinga hatua ya makundi,”.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.