Simba SC vs Nsingizini Hotspurs uongozi wa timu hiyo umebainisha kwamba utaingia uwanjani kama tmu ambayo haijafunga hivyo ni sawa na kusema matokeo yafutwa mazima ili kuongeza ushindani kwenye mchezo huo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wa Oktoba 26 Uwanja wa Mkapa wataingia kama timu ambayo haijapata matokeo kwenye mchezo wa kwanza.
Mchezo wa kwanza ugenini Oktoba 19,2025 ilikuwa Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, mabao yakifungwa na Wilson Nangu, Kibu Dennis alifunga mawili.
Ahmed amesema: “Mchezo wetu unaofuata Oktoba 26 tunaingia uwanjani matokeo yakiwa ni bilabila, hakuna kuuchukulia poa hata kidogo mchezo huu ambao ni muhimu kwetu kupata matokeo mazuri.
“Wanasimba wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao na tumeweka vingilio rafiki ambavyo vinakufanya uingie uwanjani kwa kujiamini kuipeleka timu yako hatua ya makundi,”.’
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.