Romain Folz: Tunazidi kuimarika hatua kwa hatua

ROMAIN Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema kuwa wanazidi kuimarika hatua kwa hatua kadri siku zinavyokwenda kutokana na maandalizi yanayofanyika.

Kikosi cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka leo Oktoba 16 2025 kuelekea Malawi kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Striker unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 18 2025.

Folz amebainisha kuwa kila mchezaji anafanya vizuri kwenye uwanja wa mazoezi jambo ambalo wanaamini litakuwa na mwendelezo kwa wakati ujao kuwa imara zaidi.

“Hatua kwa hatua tunazidi kuwa imara na unaona kwamba maandalizi yanaendelea na mabadiliko yanaonekana kwenye kikosi kutokana na kile ambacho tunakifanya hatua kwa hatua.

“Kikubwa ni utayari kwa kuwa mabadiliko yanahitaji muda ndivyo ambayo imekuwa kila wakati tunaona kuna maongezeko ambayo yanatokea ila haiwi ghafla, bado tupo kwenye mchakato ambao huwa unachukua muda na kwa ajili ya wakati ujao kuna kitu kizuri kinakuja,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.