KIKOSI cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz, Oktoba 16 2025 kimeanza safari kuelekea Malawi.
Ni maandalizi ya mchezo wao ujao wakiwa ugenini kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi.
Yanga SC itakakuwa na kibarua kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 18, 2025.
Huu hapa msafara wa wachezaji wa Yanga SC
Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Khomein, Israel Mwenda, Kouma, Boka, Mohamed Hussein, Dickson Job, Assinki, Bakari Nondo, Ibrahim Bacca.
Aziz Andambwile, Balla Conte, Mudathir Yahya, Duke Abuya, Doumbia, Pacome, Edmund John, Chikola, Clement Mzize, Ecua, Maxi Nzengeli, Prince Dube na Boyeli.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.