Yanga SC kuwafuata wapinzani wao CAF

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Romain Folz wapo tayari kuelekea mchezo wao ujao ugenini.

Kikosi cha Yanga SC kinatarajiwa kuwafuata wapinzani wao nchini Malawi Oktoba 16 kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wao ujao.

Mchezo wa hatua ya pili katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2025 yenye ushindani mkubwa unatarajiwa kuchezwa Oktoba 18,2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.

Mshindi wa jumla atakata tiketi kutinga hatua ya makundi ambapo mchezo wa pili wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 25, 2025.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kupata matokeo katika mechi ijayo licha ya ugumu ambao upo.

“Kuna ushindani mkubwa na hilo tunatambua hasa kwenye hatua hizi za mtoano, kikubwa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kutuombea dua malengo ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.