Sadio Mane amefunga magoli mawili na kuisaidia Senegal kufuzu kombe la Dunia la FIFA 2026 kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya Mauritania huku Ivory Coast ikifuzu moja kwa moja kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Kenya.
Senegal imemalizika kileleni mwa Kundi B alama 24 baada ya mechi 10 huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikimalizika nafasi ya pili alama 22 baada mechi 10.
Kwa upande wake Ivory Coast imemaliza kileleni mwa Kundi F alama 26 baada ya mechi 10 huku Gabon ikimaliza nafasi ya pili alama 25 baada ya mechi 10.
FT: Ivory Coast 🇨🇮 3-0 🇰🇪 Kenya
⚽ 07’ Kessie
⚽ 54’ Diomande
⚽ 84’ Amad Diallo
FT: Senegal 🇸🇳 4-0 🇲🇷 Mauritania
⚽ 45+1’ Mane
⚽ 48’ Mane
⚽ 64’ Ndiaye
⚽ 85’ Habib Diallo
FT: Morocco 🇲🇦 1-0 🇨🇬 Congo
⚽ 63’ En Nesyri
FT: Gabon 🇬🇦 2-0 🇧🇮 Burundi
⚽ 86’ Meyo Ngoua
⚽ 90-1’ Mario Lemina
DR Congo 🇨🇩 1-0 🇸🇩 Sudan
⚽ 29’ Bongonda
FT: Somalia 🇸🇴 0-1 Msumbiji
⚽ 06’ Catamo
Timu 9 kutoka Afrika zilizofuzu kombe la Dunia 2026 ni Morocco, Tunisia, Algeria, Misri, Ghana, Cape Verde, Afrika Kusini, Ivory Coast na Senegal
MSIMAMO TIMU ZILIZOMALIZA NAFASI YA PILI
🇬🇦 Gabon — pointi 19
🇨🇩 DR Congo— pointi 16
🇨🇲 Cameroon — pointi 15
🇳🇬 Nigeria — pointi 15
NB: Timu hizi zitacheza mechi ya ‘playoff’ kuanzia hatua ya nusu fainali kuwania nafasi moja ya kuwania kufuzu kombe la Dunia.