Diamond Platnumz – Nani (Official Music Video)

Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Naseeb Abdul Juma Issack, maarufu kama Diamond Platnumz, ameibua shamrashamra kubwa mitandaoni baada ya kuachia ngoma yake mpya ambayo imewapagawisha mashabiki ndani na nje ya Tanzania.

Ngoma hiyo mpya, ambayo kwa sasa imeanza kutrendi kwenye majukwaa yote ya muziki mtandaoni, imepokelewa kwa shangwe kubwa kutokana na ubunifu, sauti, na video ya kiwango cha kimataifa. Mashabiki wengi wamefurahishwa na namna Diamond alivyochanganya midundo ya Bongo Fleva na ladha za Amapiano na Afrobeat, jambo lililoongeza ubunifu na mvuto wa kipekee.

Kupitia mitandao ya kijamii, mashabiki wamekuwa wakimimina maoni chanya, wengine wakisema kuwa msanii huyo “amerudi na moto wa zamani”, huku wengine wakimtaja kama “mfalme wa muziki wa Afrika Mashariki.”