Atletico Madrid 1-1 Inter Milan, (4-2) mchezo wa kirafiki wa kimataifa

KLABU ya Atletico Madrid imepata ushindi wa penati 4-2 Inter Milan kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Oktoba 10 2025. Wababe hawa wawili walitoshana nguvu kwa kufungana 1-1 kwenye dakika 90. Atletico Madrid walianza kufungua pazia la kufunga goli dakika ya 34 kupitia kwa Carlos Martin. Inter Milan walisawazisha dakika ya 58 kupitia kwa Yann Bisseck.

Mchezo huo umechezwa nchini Libya katika bara la Afrika  Uwanja wa taifa Benghazi ulikuwa na mashabiki 42,000 walioshuhudia pambano hilo moja kwa moja. Kipa wa Atletico Juan Musso aliokoa penati mbili.

Jambo ambalo lilifurahisha mwamuzi Mustafa Al Darsi hakuongeza dakika mara baada ya dakika 90 kugota mwisho. Maamuzi yake ilikuwa moja kwa moja mshindi apatikane kwa mikwaju ya penati. Ikawa hivyo kwenye mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Afrika.

Kwenye dakika 15 za mwanzo timu zote zilikuwa zinacheza kwa uangalifu mkubwa. Dakika ya 14 Atletico Madrid walipoteza nafasi yakufunga wakiwa ndani ya 18 kupitia kwa Thiago Almada ambaye alikuwa na kipa. Dakikay a 34 ni Carlos Martin alifunga goli la kuongoza.

Carlos alipokea mpira na kuegukia lilipo lango akiwa katika hali ya kujiamini akapiga shuti. Hilo lilikuwa ni goli la ufunguzi katika kipindi cha kwanza. Lilidumu mpaka dakika ya 58 ya mchezo.

Inter Milan waliweka usawa kupitia Yann Bisseck dakika ya 58. Huo ulikuwa ni mpira wa pigo la kona ilipigwa na Henrikh Mkhitaryan. Pigo hilo lilimpa nafasi Bisseck kwenda hewani na kuushinda mpira akifunga goli la kuweka usawa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.