Singida Black Stars kazini leo, kikosi kamili hiki hapa

Singida Black Stars chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi leo Septemba 20 2025 kitakuwa kazini kwenye kete ya kwanza hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika.

Timu hiyo imetoka kutwaa ubingwa wa Kagame Cup kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal na yote kwa Singida Black Stars yalifungwa na kiungo mshambuliaji Clatous Chama.

Leo Septemba 20 kinatarajiwa kuwa uwanjani kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda saa 2:00 kwa saa za Afrika Mashariki katika Uwanja wa Kigali Pele.

Kikosi kamili cha Singida Black Stars kilichopo Rwanda hiki hapa:-

Metacha Mnata, Hussen Masalanga, Amas Obasogie, Kennedy Juma. Anthony Trabi, Mukrim Issa, Ande Koffi, Kelvin Kijili. Nickson Kibabage, Gadiel Michael, Morice Chukwu, Mohamed Damaro, Khalid Habib, Aboubakari Muhajiri huyu kutoka U 20.

Khalid Aucho, Idriss Diomande, Kwame Kekeyek, Marouf Tchakei, Clatous Chama, Deus Kaseke. Rashid Said, Lamin Jarjou,Andrew Phiri, Daud Mishamo, Elvis Rupia na Horso Muako.

Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa kimataifa na wanaamini watapata matokeo mazuri.

“Tupo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Rayon Sporta. Imani kubwa ni kupata matokeo mazuri na benchi la ufundi linafanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba tunapata matokeo mazuri.

“Kila kitu kipo sawa hivyo mashabiki wazidi kutuombea dua njema tupate ushindi kwenye mchezo wetu muhimu ambao utakuwa na ushindani mkubwa.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.