Live: Gaborone United 0-1 Simba SC

Dakika ya 87 Willson Nangu anaingia anchukua nafasi ya Ellie Mpanzu ukiwa ni mchezo wake wa kwanza katika anga la kimataifa akiwa na uzi wa Simba SC Nangu aliyeibuka hapo akitokea Ruvu Shooting.

Dakika ya 84 Shomari Kapombe anapewa jukumu la kurusha mpira

Dakika ya 83 Thomas Chideo anafanya jaribio ambalo linakuwa lenye hatari ila anakutwa kwenye mtego wa kuotea

Dakika ya 80 Chideo anafanya jaribio akiwa ndani ya 18 kwenye lango la Moussa Camara jaribio lake linakwenda nje ya lango

Dakika ya 77 Moussa Camara kipa wa Simba SC anapewa huduma ya kwanza

Dakika ya 75 Naby Camara wa Simba SC mwenye kadi ya njano anacheza faulo kwa mchezaji wa Gaborone United

Dakika ya 74 Mzamiru Yassin anapewa jukumu la kupiga mpira wa faulo anatumia mguu wake wa kulia

Dakika ya 72 Mzamiru Yassin anapewa jukumu la kupiga faulo anamtafuta Shomari Kapombe pembeni kabisa

Kadi nyekundu

Dakika ya 68 kocha msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola anaonyeshwa kadi nyekundu

Mabadiliko kwa Simba SC

Kibu Dennis anaingia anatoka Seleman Mwalimu

Mzamiru Yassin anaingia dakika ya 65 anatoka Kante

Dakika ya 63 Seleman Mwalimu anacheza faulo, Moussa Camara anapewa huduma ya kwanza dakika ya 64

Dakika ya 62 Jean Ahoua anajaribu kukokota mpira kuelekea lango la Gaborone mpira huo unapokwa na beki wa Gaborone.

Dakika ya 60 nyota wa Simba SC Naby Camara anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo mchezo wa Gaborone United

Dakika ya 58 Shomari Kapombe anaokoa hatari

Dakika ya 57 Camara anachezewa faulo na anapiga faulo dakika ya 57

Dakika ya 56 Rushine anachezewa faulo inapigwa na Camara Moussa

Dakika ya 55 Gaborone United wanatengeneza nafasi nzuri ambayo inapotea bila faida baada ya safu ya ulinzi ya Simba SC kufanya makosa

Dakika ya 53 Gaborone wanapiga kona baada ya Mligo kuokoa hatari iliyokuwa inakwenda kwa Camara

Dakika ya 49 Kalagho anafanya jaribio kuelekea lango la Simba SC linakwenda nje ya lango

Dakika ya 48 Ellie Mpanzu jaribio lake linakwenda nje ya lango

Dakika ya 47 Seleman Mwalimu anachezewa faulo

Dakika ya 45 Jean Ahoua anapeleka mashambulizi Gaborone, Maema anafanya jaribio linaokolewa na mlinda mlango wa Gaborone

Kipindi cha pili kimeanza

Dakika 45 zinakamilika

Gaborone United 0-1 Simba SC

Dakika ya 45 Kante anafanya faulo karibu kabisa na eneo la 18 kwa Simba SC alipo Camara

Dakika ya 45 Johnson anapiga faulo ambayo inakwenda nje kidogo ya lango la Simba SC

Dakika ya 42 Anthon Mligo anaokoa mara mbili na anapewa jukumu la kurusha mpira, dakika ya 43 Alfred anafanya jaribio linakwenda langoni na kuokolewa na Camara

Dakika ya 40 Legho anapeleka mashambulizi Simba SC, Ellie Mpanzu anacheza faulo dakika ya 41 Motsi Johson anapewa jukumu la kupiga faulo hiyo inaokolewa na Rushine

Dakika ya 39 Seleman Mwalimu ambaye yupo Simba SC kwa mkopo akiwa ndani ya 18 anakwama kuwa na utulivu kwa pasi ya Mpanzu iliyomfikia.

Dakika ya 38 Jose anarusha mpira kuelekea lango la Simba SC, Thabo Musogore anaokoa hatari langoni

Dakika ya 37 Mpanzu anapiga pasi fupi kumtafuta Maema inakuwa ni pasi mkaa haifiki kwenye eneo husika na mpira unatoka nje

Dakika ya 35 Ibrahim anapeleka mashambulizi mbele kwa Simba SC, Naby Camara anaokoa hatari

Dakika ya 34 Anthony Mligo anapewa jukumu la kurusha mpira, dakika ya 35 Ahoua anapoteza pasi aliyopewa na Kapombe

Dakika ya 33 nahodha Shomari Kapombe anarusha mpira kwa Jean Ahoua

Dakika ya 32 Jean Ahoua anapiga kona fupi kwa Shomari Kapombe

Dakika ya 32 Chamou anapiga faulo

Dakika ya 31 Naby Camara anachezewa faulo beki Alpherd Velaph anaonyeshwa kadi ya njano, inapigwa na Chamou Karaboue

Dakika ya 30 Camara anaanzisha pasi ndefu, Rushine anacheza faulo, Kagaswane anatafuta lango la Simba SC

Dakika ya 28 Lwamagi anachezewa faulo na Gaborone wanapata pigo huru nje kidogo ya 18, Camara anawapanga wachezaji wa Simba SC na Johson anapiga faulo dakika ya 29 ambapo Gaborone wanakutwa kwenye mtego wa kuotea

Dakika ya 27 beki Rushine anapiga mpira mrefu ambao unakwenda moja kwa moja kwa mlinda mlango wa Gaborone, Thabo Musugore.

Dakika ya 26 Camara anaokoa mpira na kuanza kumpa Rushine, Thabo anafanya jaribio kuelekea lango la Simba SC halileti matunda

Dakika ya 24 Naby Camara anacheza faulo kwa mchezaji wa Gaborone United

Dakika ya 21 Neo Maema anachezewa faulo na Tatenda Gora ambaye yupo katika timu ya taifa ya Botswana anakuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 20 Thabo kipa wa Gaborone anaanzisha mashambulizi kuelekea lango la Simba SC baada ya Chamou kutoa nje mpira, Mpanzu aafanyiwa faulo

Dakika ya 19 Naby Camara anarudisha mashambulizi kwa Camara

Dakika ya 18 kiungo Kagaswane anafanya jaribio kuelekea lango la Simba SC linakwenda nje ya lango

Gooool Simba SC

Dakika ya 15 Ellie Mpanzu anapachika goli la kuongoza kwa Simba SC ni pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 akimalizia krosi iliyopigwa na beki Shomari Kapombe

Dakika ya 13 Ellie Mpanzu anakutwa kwenye mtego wa kuotea

Dakika ya 10 Thabo mlinda mlango wa Gaboro United anapewa huduma ya kwanza

Dakika ya 7 nyota wa Gaborone anachezewa faulo na kupewa huduma ya kwanza ni Lwamagi

Dakika ya 5  Gaborone wanafanya jaribio la hatari ndani ya 18 linaokolewa na Moussa Camara

Desemba 2 2023 Simba SC ilicheza kwenye Uwanja huu na kutoshana nguvu bila kufungana na Jwaneng Galaxy

Dakika ya tatu Jackson anarusha mpira kuelekea lango la Simba SC

Dakika ya pili Ellie Mpanzu pasi yake inakuwa mkaa

Dakika ya kwanza Jean Ahoua anafanya jaribio la hatari kwa Simba SC linakwenda nje ya lango.

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Botswana Uwanja wa Francistown ikiwa ni hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.