
SIMBA SC NDANI YA DAR KAMILI KWA SIMBA DAY SEPTEMBA 10
KIKOSI cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kimewasili salama Jijini Dar es Salaam alfajiri ya saa 11 kikitokea Misri ambako kiliweka kambi ya msimu ujao wa 2025/26. Baada ya kuwasili kikosi cha Simba SC kinatarajia kuanza maandalizi mapema kuelekea kwenye mchezo wa Simba Day unaotarajiwa kuchezwa Septemba 10 2025 Uwanja wa Mkapa….