Hemed Suleman, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema watafanyia kazi makosa yaliyopita kuwa imara zaidi huku akibainisha kuwa ni ngumu kucheza na timu ambayo haina chakupoteza.
Tanzania Agosti 16 2025 mchezo wa CHAN 2024 ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Afrika ya Kati 0-0 Tanzania. Licha ya matokeo hayo Tanzania ina tiketi ya robo fainali huku wapinzani wao wakiishia hatua ya makundi.
“Nafikiri ilikuwa mechi nzuri. Tangu mwanzo nilikuwa ninasema kwamba utakuwa mchezo mgumu. Ninawashukuru wachezaji wamepambana. Tutafanyia kazi makosa kuwa bora zaidi hatua ya robo fainali.
“Nafikiri katika makundi yote hakuna Kundi jepesi. Makundi yote ni magumu. Ninaangalia makundi yote na acha tuangalie nani tunakwenda kukutana naye. Sisi tupo tayari kwa ajili ya timu yoyote na hata ukiangalia kwenye kundi letu nalo ni gumu.
“Kuna maendeleo ambayo yanatokea kilasiku timu inazidi kuwa imara.Tulikuwa tunajaribu kuhakikikisha kuwa tunakuwa imara kwenye safu ya ushambuliaji. Huu mpira kuna mengi ambayo yanatokea, siwezi kulaumu sana kutokana na matokeo.
“Jambo la msingi tulitengeneza nafasi tukakosa. Mpira upo hivyo kuna kitu ambacho kinaonekana hakijaenda sawa. Huko tunakoenda tunahitaji matokeo na ninafikiri tutakaa sawa kwenye mechi zijazo. Ni ngumu kucheza na timu ambayo haina cha kupoteza.
Katika mchezo huo kiungo Feisal Salum alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Ni tuzo yake ya pili kwenye mashindano ya CHAN 2024.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.