VIPERS SC YAMSAJILI WINGA MNIGERIA ODILI CHUKWUMA KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

Mabingwa wa Ligi Kuu Uganda, Vipers Sc wamethibitisha kumsajili winga, Mnigeria Odili Chukwuma kwa mkataba wa miaka miwili utakaombakisha klabuni hapo mwisho wa msimu wa 2026/27.

Chukwuma (23) raia wa Nigeria anajiunga na Mabingwa hao mara 7 wa Ligi Kuu Uganda kutoka klabu ya Police Fc ya Rwanda.

Msimu uliopita Chukwuma alifunga magoli matano na kusaidia ‘assists’ mengine 8 akiisaidia Polisi Fc kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Rwanda wakiwa na pointi 48.

Chukwuma ambaye pia amewahi kuichezea Bugesera Fc ya Rwanda anakuwa usajili wa nne wa Vipers Sc baada ya mshambuliaji Mark Yallah raia wa Liberia, kiungo Kevin Dasylva Bady kutoka DRC na kiungo Enock Ssebaggala raia wa Uganda.