KIBU DENNIS WA SIMBA SC 2024/25 MABAO MANNE

SIMBA SC katika anga la kimataifa msimu wa 2024/25 imegotea nafasi ya pili kwa kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Katika dakika 180, Simba SC ilifungwa jumla ya mabao 3-1, bao la kufutia machozi kwa Simba SC lilifungwa na Joshua Mutale mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Kibu Dennis ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa katika ubora kwenye mashindano ya kimataifa kwa kufunga mabao muhimu katika mechi za ushindani Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika Ligi Kuu Bara 2024/25 haukuwa msimu bora kwa Kibu D kutokana na namba kuwa chini hasa katika eneo la kutengeneza pasi za mwisho.

Kibu D alitoa jumla ya pasi nne na kufunga mabao manne na kasi katika kufunga mabao ilianza kuonekana katika mzunguko wa pili.

Rekodi zinaonyesha kuwa amecheza jumla ya mechi 24 za ligi ya NBC akifunga mabao manne na kutoa pasi nne hivyo kahusika katika mabao 8 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.