CR 7 ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA JOTA

MSHAMBULIAJI bora wa muda wote kwa sasa raia wa Ureno Cristiano Ronaldo ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Diogo Jota na kaka yake Andre Silva.

Ulimwengu wa mpira kwa sasa unaomboleza kufuatia kutangulia mbele za haki kwa kijana huyo mwenye miaka 28. Kijana huyo alikuwa kwenye safari kuelekea kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 ndani ya Klabu ya Liverpool.

Ronaldo ameonesha masikitiko yake akisema ni hivi majuzi tu walikuwa wote kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno lakini pia ni juzi tu Jota ameoa hii inakuwa ngumu kuipokea kuwa leo amefariki.

Nahodha huyo wa Ureno ametuma salamu za pole kwa familia ya Jota na wapenda soka ulimwenguni kwa msiba huo mzito wa Jota na Adre.

Liverpool wamebainisha kuwa wapo bega kwa bega na familia kuhusu suala hilo na wao walipokea taarifa kuhusu kutangulia mbele za haki kwa Jota ambaye alikuwa anavaa jezi namba 20.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka kwa msaada wa mtandao, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.