MSHINDI WA VAZI BORA APONGEZA UZINDUZI WA HEINEKEN SILVER

Mshindi wa vazi bora katika kipengele cha “Silver Futuristic” ameibuka na kitita cha shilingi milioni 2, ametoa pongezi kwa uzinduzi wa kinywaji kipya cha Heineken Silver ambacho amesema ni laini kwa ladha lakini kina nguvu isiyo na mpinzani sokoni.

Uzinduzi huo wa kuvutia ulifanyika usiku wa kuamkia Jumapili, Juni 22, 2025, ndani ya viunga vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, ukikusanya zaidi ya wageni 400.

Miongoni mwao walikuwepo mastaa wakubwa wa Bongo, influencers maarufu, content creators wa kizazi kipya, na mashabiki wa burudani kutoka kona mbalimbali za jiji.

Tukio hilo liligubikwa na mvuto wa kisasa, mitindo ya hali ya juu, burudani ya kiwango cha kimataifa na muonekano wa kipekee likiwa ni ishara rasmi ya kuingia kwa Heineken Silver kwenye soko la Tanzania kwa kishindo.
Kwa sasa, kinywaji hicho kimeanza kupokewa kwa shangwe mitaani kote nchini, kikitambulika kama chaguo jipya la watu wenye ladha ya kipekee na maisha ya kisasa.