MKALI anayekimbiza kunako Bongo Fleva, Mbwana Yusuf Kilungi almaarufu kama Mbosso Khan, ametikisa tena anga ya muziki kupitia ngoma yake mpya “Aviola (Bonge la Dada).”
Wimbo huu ambao tayari unafanya vizuri mitandaoni na kwenye vituo vya redio, umekuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa burudani kutokana na mdundo wake wa kuvutia, mashairi yenye hisia kali, pamoja na uimbaji wa kipekee wa Mbosso.
Mashabiki wake wameipokea ngoma hiyo kwa mikono miwili, wakisema ni “bonge la kazi” inayothibitisha hadhi ya Mbosso kama mmoja wa wanamuziki wa kiwango cha juu kabisa Afrika Mashariki.