Baada ya dakika 90 kukamilika mzunguko wa 29 jumla yamefungwa mabao 22 kutoka katika viwanja 8 tofautitofauti msimu wa 2024/25 kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.
Kutoka viwanja 8 ni Uwanja wa Majaliwa pekee dakika 90 ziligota mwisho bila kupatikana kwa bao kwa timu zote mbili ambapo ubao ulisoma Namungo FC 0-0 Kagera Sugar wababe hawa waligawana pointi mojamoja.
Timu mbili zilikomba pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0, ilikuwa Pamba Jiji 1-0 JKT Tanzania bao la ushindi likiwa ni mali ya Zabona Mayombya ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Coastal Union 1-0 Fountain Gate kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga pointi tatu zikiwa ni mali ya Coastal Union. Dodoma Jiji ilipoteza pointi tatu kwa kushuhudia ubao ukisoma Dodoma Jiji 1-2 Singida Black Stars. Mashujaa waligawana pointi mojamoja na KMC kwa ubao kusoma 1-1.
Ushindi wa 5G kwa timu tatu ambazo zipo ndani ya tatu bora kwenye msimamo, Yanga SC, Simba SC na Azam FC. Timu mbili zilikuwa ugenini huku Azam FC ikiwa nyumbani, Uwanja wa Azam Complex.
Timu tatu ambazo zipo ndani ya tatu bora zilipatq ushindi wa mabao 5-0, ni Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC, Azam FC 5-0 Tabora United na KenGold 0-5 Simba SC.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.