FAINALI CRDB FEDERATION CUP KUPIGWA JUNI 29 2025

MCHEZO wa fainali ya CRDB Federation Cup kati ya Yanga SC vs Singida Black Stars umepelekwa mbele mpaka Juni 29 2025, Uwanja wa New Amaan saa 2:15 usiku.

Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Juni 28 2025, mabadiliko hayo yametokana na uwepo wa mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Yanga SC vs Simba SC.

Mchezo wa Kariakoo Dabi awali ulitarajiwa kuchezwa Juni 15 2025, umepelekwa mbele mpaka Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa kwa wababe hao kukutana kusaka pointi tatu.

Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Yanga SC ilifika hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Inakwenda kukutana na Singida Black Stars ambayo iliwafungashia virago Simba SC kwenye hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.