KITUO kinachofuata kwa Simba SC ndani ya Ligi Kuu Bara ni mchezo dhidi ya KenGold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni mzunguko wa pili.
Simba SC mchezo wake wa mwisho kwenge ligi ilikuwa dhidi ha Singida Black Stars uliochezwa Uwanja wa KMC Complex na mwisho ubao ulisoma Simba SC 1-0 Singida Black Stars.
Bao pekee la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji Steven Mukwala ambaye alitumia pasi ya Jean Ahoua kiungo mshambuliaji mwenye jumla ya pasi 8 ndani ya ligi namba nne kwa ubora.
KenGold kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 28 msinu wa 2024/25.
Inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili pointi 72 baada ya mechi 27 ikiwa inapambania kutwaa ubingwa mbele ya Yanga SC ambao ni vinara wenye pointi 73.
Kwa upande wa mabao Simba SC imefunga mabao 63 inakutana na KenGold ambayo imefunga jumla ya mabao 22.
Mchezo ambao ulitarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 ambao ulikuwa ni Kariakoo Dabi mchezo namba 184 umepelekwa mbele na sasa utachezwa Juni 25 kwa wababe hawa kukutana uwanjani katika msako wa pointi tatu muhimu.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.