Klabu ya Simba kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, imeeleza kuwa imeruhusiwa kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa na vingine vyote vilivyopo chini ya wizara bila ya kukwamisha kwa namna yoyote matumizi ya viwanja hivyo.
Simba imeposti barua kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inayoonesha taarifa ya kuruhusiwa kutumia uwanja huo Juni 14, 2025 kwa ajili ya mazoezi rasmi ya timu.