BODI YA LIGI KUTOA TAARIFA KUHUSU KARIAKOO DABI MUDA WOWOTE

Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Karim Boimanda ameweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 yapo vizuri na kuna taarifa nyeti na muhimu zitatolewa muda wowote kuanzia sasa.

Yanga SC ni wenyeji wa mchezo huo namba 184 ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo watakipiga dhidi ya Simba SC ambao katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza pointi tatu muhimu ubao uliposoma Simba SC 0-1 Yanga SC.

Boimanda ameweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri kutokana na ukubwa wa mchezo ambao unatoa taswira ya ligi ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

“Maandalizi yapo vizuri lakini pia ni vizuri nikitoa taarifa kuwa kuna baadhi ya taarifa nyeti na muhimu kwa ajili ya mchezo huo zitatolewa muda wowote kuanzia sasa hivyo zitakuwa zinakwenda kutamatisha kuhusu maandalizi ya mchezo nadhani wadau wanapaswa kusubiri kusikia kutoka bodi ya ligi kusikia kuhusunia na mchezo huo.

“Tumekuwa tukisisitiza kuwa maandalizi yanaendelea. Tunaamini kwamba wadau wengine zikiwemo hizo timu mbili Yanga SC na Simba SC wanaendelea na maandalizi mchezo ambao ni mkubwa mchezo namba 184 ambao ni kioo cha ligi yetu mchezo ambao umekuwa ukivuta hisia za watu wengi.

“Ni matumaini yetu kwamba wadau wote wanaendelea na maandalizi yao. Na kwamba kwa maana ya ujumbe kutoka bodi ya ligi ni kwamba ili tukio hili kubwa lifane kila mmoja lazima ashiriki kwa ukamilifu kwa ajili ya tukio hili ili kufikia siku tukiwa tayari kubwa ambalo limekuwa likivutia hata watu wa nje kwa ajili ya mchezo huu muhimu.

“Kuna baadhi ya taarifa muhimu zitatolewa muda mfupi kuanzia sasa zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni ikiwa ni kama vile maofisa wa mchezo, kwa maana ya waamuzi, viingilio masuala ya uuzwaji wa tiketi zitatolewa hivi karibuni. Kuhusu mechi za raundi mbili za mwisho Boimanda ameweka wazi kuwa mchezo wa raundi ya 29 Juni 18 na raundi ya 30 Juni 22.

“Viwanja vyote ambavyo awali kulikuwa na changamoto tuliwasiliana na vilabu vyote kwa ajili ya maboresho na kwa asilimia kubwa tayari vimekamilika. Michezo ya raundi mbili ya 29 na 30 kila kitu kipo sawa na tusubiri burudani yakutamatisha msimu wa 2024/25.

Source: Azam TV

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.