SIMBA SC WAULIZIA RIPOTI YA KARIAKOO DABI KUYEYUKA

UONGOZI wa Simba SC umetoa taarifa kwa umma kuwa mchezo wao wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC unaotarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 upo kama ulivyopangwa.

Taarifa ambayo imetolewa mapema Juni 10 2025 na Simba SC imeeleza kuwa Klabu ya Simba inatoa taarifa kwa Wanachama, wapenzi na umma kuwa mchezo nambari 184 dhidi ya Yanga SC uliopangwa kufanyika Juni 15 2025 upo kama ulivyopangwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa inawasihi mashabiki wasihadaike na kelele za mtaani wale ambao walinunua tiketi za mechi ya Machi 8 2025 wazitunze kwa ajili ya matumizivya mchezo huo na we ambao hawajanunua tiketi wajiandae kununua baada ya tangazo ka Bodi ya ligi.

Simba SC ambao watakuwa wageni katika mchezo huo wamekuja na sera inayosema kuwa : “Twendeni tukaujaze Uwanja wa Mkapa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa inafahamika wazi kuwa Ligi Kuu ya NBC inajumuisha timu 16 na si ligi ya timu moja. Kwa mujibu wa taratibu kabla ya kuanza msimu vilabu vyote 16 hushiriki vikao na kutoa mapendekezo ya kuboresha kanuni na taratibu ili kuimarisha ligi hivyo wenye hoja wafuate taratibu husika.

Simba SC wameiomba Bodi ya Ligi na TFF watoe hadharani ripoti ya uchunguzi juu ya wale wote waliohusika kuharibu mechi ya ligi jioni ya Machi 7 2025 na wachukuliwe hatua stahiki na mamlaka husika.

Wamemaliza kwa kuandika kwamba kutotolewa kwa ripoti na kutochukuliwa hatua kwa wanaoendelea kuchochea ghasia ni sawa ba kulinda uharamia katika mpira ambao unatia dosari mafanikio yaliyopo katika tasnia ya mpira wa miguu nchini kwa sasa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.