BEKI wa zamani wa Yanga SC Gift Fred ambaye alishindwa kupata namba kikosi cha kwanza na kupewa Thank You anatajwa kupata dili nono kwa ajili ya changamoto mpya.
Gift Fred anakaribia kujiunga na Klabu ya KCCA ya nchini Uganda katika msimu ujao wa 2025/26 kwa ajili ya kutimiza majukumu yake.
Gift anakwenda kujiunga na KCCA akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mkopo St George ya nchini Ethiopia kumalizika.
Ni Yanga SC ya Tanzania ilimpeleka beki huyo kwa mkopo St George baada ya kutovutiwa na kiwango chake akishindwa kuwapa ushindani Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.
Gift alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 2023 alikwama kuonyesha uwezo katika mechi za ushindani.
Kwa sasa kwenye eneo la beki wa kati chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga SC ni Dickson Job ambaye huyu anatajwa kuwa ataongezewa kandarasi nyingine kubaki ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.