ALIYEKUWA beki wa kati wa Yanga, Gift Fred anakaribia kujiunga na Klabu ya KCCA ya nchini Uganda katika msimu ujao.
Gift anakwenda kujiunga na KCCA kama mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mkopo St George ya nchini Ethiopia kumalizika.
Yanga ndiyo iliyompeleka beki huyo kwa mkopo St George katika msimu wa 2024-2024 baada ya kutovutiwa na kiwango chake akishindwa kuwapa ushindani Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.