BRUNO FERNANDES AKATAA MAMILIONI YA AL HILAL, AAMUA KUSALIA ULAYA

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes ametupilia mbali ofa nono kutoka Al Hilal ya Saudi Arabia kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo ya Ligi kuu ya Saudi Pro huku akitaka kuendelea kusakata kabumbu barani Ulaya.

Bruno (30) raia wa Ureno amefanya maamuzi ya kukataa ofa nono ya mshahara wa pauni laki 7 kwa wiki (takribani Tsh bilioni 2.55) huku akichagua kusalia Manchester United, timu iliyomaliza nafasi ya 15 msimu uliomalizika huku ikipoteza mchezo wa fainali ya Europa League.