PROFESA JANABI ASHINDA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi leo Mei 18, 2025 ameibuka kidedea katika uchaguzi wa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.

Katika uchaguzi uliofanyika Geneva nchini Uswisi, Janabi alikuwa akichuana na wenzake wanne, Dk. N’da Konan Yao wa Ivory Coast, Dk Drame Lamine wa Guinea, Dk Boureima Sambo wa Niger na Prof. Mijiyawa Moustafa kutoka Togo.

Sasa ni rasmi Tanzania imetoa mkurugenzi mwingine katika nafasi hiyo, baada ya awali, Dk. Faustine Ndugulile aliyeshinda, kufariki dunia kabla hajaanza kutumikia rasmi nafasi hiyo.