LIGI Kuu Tanzania Bara inazidi kushika kasi ikiwa ni mzunguko wa pili kasi inazidi kuendelea ambapo ni Jean Ahoua anaongoza chati kwenye eneo la utupiaji wa mabao.
Kufunga hat trick mbele ya Pamba Jiji, Mei 8 2025 kumempa nafasi kumshusha kinara mzawa Clement Mzize ambaye ana mabao 13 ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Ahoua ndani ya ligi katupia jumla ya mabao 15 huku kikosi cha Simba kikiwa kimetupia jumla ya mabao 60 namba mbili kwa timu yenye mabao mengi ndani ya ligi ikiwa inaongozwa na Yanga SC yenye mabao 68.
Kwenye mabao hayo Ahoua kafunga kwa Free Kikc mabao mawili ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba na Pamba Jiji Uwanja wa KMC Complex.
Kwa mapigo ya penalti ni mabao 6 kafunga na alifungua ukurasa kwenye mapigo ya penati dhidi ya Dodoma Jiji ilisababishwa na Mohamed Hussen na penati ya sita dhidi ya Pamba Jiji ilisababishwa na Joshua Mutale.
Ahoua kwenye mabao 15 ambayo ametupia ni mabao 14 kafunga kwa mguu wa kulia bao moja kwa pigo la kichwa dhidi ya Pamba Jiji.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.