JKT TANZANIA YATUMA UJUMBE MZITO YANGA SC CRDB FEDERATIN CUP

OFISA Habari wa JKT Tanzania, Masua Bwire amesema kuwa watapambana kwenye mashindano yote ambayo wanashiriki kupata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na mchezo wao wa CRDB Federation Cup wakiwa hatua ya nusu fainali.

JKT Tanzania kwenye CRDB Federation Cup imetinga hatua ya nusu fainali na inatarajiwa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya fainali dhidi ya mabingwa watetezi Yanga SC.

Mei 16-18 mechi za hatua ya nusu fainali zinatarajiwa kuchezwa ambapo Yanga SC itakuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkwakwani Tanga na mshindi wa mchezo atakutana na Simba SC ama Singida Black Stars ambao mchezo wao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.

Masau Bwire amesema kuwa nguvu hawana mashaka na mechi zote ambazo zipo mbele yao ikiwa ni nusu fainali ya CRDB Federation Cup kwa kuwa wapo imara na maandalizi yanaendelea.

“Sisi tupo imara na nguvu kubwa ni kuona kwamba tunashiriki mashindano ya kimataifa, wapinzani wetu niseme kwamba watatupisha, hao hao ambao tutakutana nao hakika safari hii watatupisha tunahitaji kushiriki mashindano ya kimataifa.

“Wachezaji na benchi la ufundi lipo tayari kwa ajili ya mechi zetu na kwenye mechi za ligi ambazo zimebaki tutapambana kuona kwamba tunapata ushindi.”

Mchezo uliopita kwa Ruvu Shooting ilikuwa ni Mei  5 baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 0-1 Simba SC, bao la ushindi lilifungwa na Fabrince Ngoma dakika ya 45 na alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.