SINGIDA Blac Stars, walima alizeti wamekomba pointi tatu mazima kwa ushindi mbele ya nyuki wa Tabora, Tabora United kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Liti, Singida.
Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na Victorean Adebayo aliyefungua pazia la mabao dakika ya 21, Jonathan Sowah katupia mabao mawili ilikuwa dakika ya 52 na 86.
Kwenye mechi tano za hivi karibuni, Tabora United haijawa kwenye mwendo mzuri ndani ya mzunguko wa pili kusaka pointi tatu muhimu ambapo kila mchezo ilikuwa inaangusha pointi tatu muhimu.
Mchezo wao dhidi ya Mashujaa walipoteza ugenini kwa kufungwa mabao matatu na leo Aprili 19 2025 ikiwa ugenini imepoteza kwa kufungwa mabao 3-0 na kupoteza pointi tatu kwa mara nyingine tena.
Mechi zilizopita kwa Tabora United ilikuwa namna hii matokeo yao:-
Tabora United 1-2 JKT Tanzania, Tabora United 0-3 Yanga, Pamba 1-0 Tabora United
Mashujaa 3-0 Tabora United kete ya tano kupoteza ni Singida Black Stars 3-0 Tabora United.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.