DIOGO JOTA APELEKA KILIO, POINTI 12 UBINGWA HUO

KWENYE Merseyside Derby, Liverpool wamekomba pointi tatu mazima mbele ya Everton katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Anfield wakiendeleza kampeni yao kuwinda ubingwa wa Ligi Kuu England.

Shukrani kwa Diogo Jota ambaye alifunga bao la ushindi kwenye mchezo huo kipindi cha pili dakika ya 57 likafumu mpaka mwisho wa mchezo.

Pointi 73 wanafikisha Liverpool wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi, ushindi ni katika mechi 22, wamepoteza mchezo mmoja na kuambulia sare katika mechi 7.

Chini ya Kocha Mkuu, Arne Slot, Liverpool imekuwa katika mwendo mzuri na sasa wanahitajika kushinda mechi nne ambazo ni pointi 12 kujihakikishia nsfasi ya kutwaa ubingwa.

MANCHESTER CITY NAO

Manchester City 2-0 Leicester City, bao la mapema dakika ya 2 likipachikwa na Jack Grealish na bao ka pili likipachikwa na Omar Marmoush dakika ya 28 huku nyota wa City, Nicolas Gonzalez akionyeshwa kadi ya njano dakika ya 80.

Upande wa Leicester City ni James Justin dakika ya 71, Luke Thomas dakika ya 76 na Oliver Skipp dakika ya 89 hawa walionyeshwa kadi ya njano kila mmoja Uwanja wa Etihad

Matokeo hayo yanaifanya City kufikisha pointi 51 nafasi ya 4 kwenye msimamo baada ya mechi 30 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 57 ikiwa imepata ushindi katika mechi 15 poteza 9, sare 6.

Leicester City nafasi ya 19 ina pointi 17 baada ya mechi 30, ushindi ni kwenye mechi 4 poteza mechi 21 na sare 5 msimu wa 2024/25.

DARAJANI KUNA KAZI APRILI 3

Chelsea watakuwa Uwanja wa Stamford Bridge kuvaana na Tottenham katika mchezo wa Ligi Kuu England ikiwa ni wiki ya 30 na wanapewa asilimia 57 za ushindi wakiwa nyumbani huku Tottenham wakipewa asilimia 21.

Kwenye msimamo Chelsea ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 49 baada ya mechi 29 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 53 na ukuta umeruhusu mabao 37.

Wapinzani wao Tottenham wapo nafasi ya 14 wakiwa na pointi 34 baada ya mechi 29 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 55 ukuta ukiruhusu mabao 43.

Kutoka kikosi cha Chelsea kinara wakutupia mabao ni Cole Palmer ambaye ametupia mabao 14 kibindoni na mkali wa pasi za mwisho za mabao kwa wababe hawa wawili ni Son Heung-min wa Tottenham akiwa ametoa pasi 9.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, mtandao, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.