CLEMENT Mzize, mchezaji bora Desemba amewakimbiza wachezaji wenye rekodi kutokana na kusepa na tuzo hiyo mbele ya mastaa wenye rekodi zao ndani ya NBC.
Kwenye mechi nne ambazo alicheza, Mzize alifunga mabao manne na kutoa pasi tatu za mabao akikomba dakika 288 na Yanga ilikuwa nafasi ya tatu ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC ikapanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Alikuwa akiwania tuzo na Feisal Salum kinara wa pasi za mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara yupo zake Azam FC akiwa ametoa pasi 9 za mabao na kafunga mabao manne, katika hayo mabao matatu alifunga kwa mapigo ya penaltI.
Nyota mwingine alikuwa ni Prince Dube huyu mshambuliaji anayeshikilia rekodi ya kuwa wa kwanza kufunga hat trick ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25.
Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa Kombe la CRDB Federation unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex Januari 25 2025 saa 10:00 jioni.
Katika mchezo huo mzunguko kiingilio ni 10,000 na VIP ni 20,000 kuwashuhudia mastaa wa Yanga na dhidi ya Copco FC wakiwania ushindi kwenye mchezo huo wa mtoano.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.