TAARIFA rasmi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya nne (4) kwa ubora barani Afrika.
Wakati ikiwa ni namba nne kwa ubora barani Afrika imekuwa ya 57 duniani kwa mwaka 2024 hii ikiwa inamaanisha kwamba ushindani unazidi kukua kila iitwapo leo ndani ya ardhi ya Tanzania kwenye upande wa michezo.
Ligi hiyo imepanda kwa nafasi mbili (2) kutoka nafasi ya sita (6) mwaka 2023 ikizipiku Ligi za Afrika Kusini na Tunisia.
Ligi namba moja ni ile ya Misri, namba mbili ni Morocco na tatu ni ligi ya Algeria hivyo Tanzania imepanda mpaka nafasi ya nne kwa ubora.
Ipo wazi kwamba ni timu mbili katika anga la kimataifa zilitinga hatua ya makundi ambazo ni Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba imeendelea na safari yake ambapo ipo hatua ya robo fainali huku Yanga ikigotea hatua ya makundi ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nafasi ya tatu na pointi 8 kutoka kundi A.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.