LIGI KUU BARA YASHIKA LIKI NAMBA NNE KWA UBORA AFRIKA
Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya nne (4) kwa ubora barani Afrika na ya 57 duniani kwa mwaka 2024. Ligi hiyo imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya sita mwaka 2023 ikizipiku Ligi za Afrika Kusini na Tunisia…