YANGA YAWAPIGIA HESABU WAARABU KWA MKAPA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga wameweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya MC Alger unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Yanga imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal ikiandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi kwa Al Hilal ambao ni vinara wa kundi A kwenye hatua za makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga dakika ya 7 akitumia pasi ya beki wa kupanda na kushuka likiwa ni bao la mpema zaidi kufungwa na Yanga kwenye hatua za kimataifa kwenye makundi msimu wa 2024/25.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo na kikubwa ambacho wanahitaji ni kupata pointi tatu kutinga hatua ya robo fainali Afrika.

“Tunamchezo mkubwa na muhimu mbele yetu dhidi ya MC Alger, tutakuwa nyumbani hivyo ni jambo la msingi kwa mashabiki kulitambua hilo na hii mechi ni yetu sote sio wachezaji peke yao hapana kazi kubwa kwenye kutafuta matokeo inafanyika kwa ushirikiano.

“Katika kila hatua tumekuwa pamoja hivyo ni mwendelezo wakuona kwamba sasa tunafanya vizuri na kupata matokeo kwenye mchezo wetu muhimu tukiwa Uwanja wa Mkapa inawezekana mashabiki tujitokeze kwa wingi.”

Yanga ina pointi 7 ikiwa nafasi ya tatu inakutana na wapinzani wao MC Alger nafasi ya pili na pointi zao ni 8 hivyo namna pekee ya Yanga kutinga hatua ya robo fainali ni ushindi hakuna chaguo lingine.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.