YANGA WATUMA UJUMBE HUU KIMATAIFA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema kuwa lazima waonyeshe ukuaji wao kwa kuongeza umakini kwenye mchezo dhidi ya Al Hilal ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga inasaka pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika imekusanya pointi nne kwenye makundi ikiwa nafasi ya tatu inakutana na vinara Al Hilal wenye pointi 10 kibindoni.

Mchezo uliopita Yanga ilivuna pointi tatu muhimu kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe, mabao mawili ya Clement Mzize na bao moja la Aziz Ki.

Ramovic amesema: “Lazima tuonyeshe ukuaji wetu, tuchukue kila nafasi kwa umakini na tuwe na uthubutu wa kushambulia ili tuweze kutengeneza nafasi ya ushindi. Wanacheza kwa kasi na tunapaswa kuwa tayari kukabiliana nao.”

Kwa upande wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo na malengo ni kuona kwamba wanapata pointi tatu muhimu.

“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu kwa upande wetu tuna lengo moja na lengo hilo ni kuendelea kwenye hatua inayofuata. Ili kufanikisha hilo, tunapaswa kucheza kwa bidii zaidi hili ni jukumu letu na tutafanya kila kitu kuhakikisha tunafanikiwa.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.