SIMBA kwenye mechi tano za kimataifa safu yake ya ushambuliaji imefunga katika mechi hizo katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
Mbele ya Bravos Leonel Ateba amefunga bao dakika ya 69 akisawazisha bao walilofungwa na Abdenego dakika ya 13 wakifungua ukurasa wa kutinga hatua ya robo fainali.
Simba inafikisha pointi 10 kwenye hatua ya makundi kinara ni Constatine kete ya mwisho Simba itakuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya vinara wa kundi.
Kwenye mchezo wa leo kipindi cha kwanza ziliongezwa dakika tatu na kipindi cha pili ziliongezwa dakika 5 hivyo ni dakika 8 ziliongezwa katika anga la kimataifa.
Kiungo Yusuph Kagoma alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo wa leo aligotea dakika ya 45 nafasi yake ilichukuliwa na Mavambo.
Ateba naye hakusepa na dakika 90 licha ya kufunga bao moja dakika ya 69 likiwa ni bao lake la kwanza hatua ya makundi aligotea dakika ya 88 nafasi yake ikachukuliwa na Mashaka Valentino.
Simba wametinga hatua ya makundi wakiwa na pointi 10 vinara ni Constatine wenye pointi 12 hawa ni vinara na Bravos ni pointi 7 nafasi ya tatu, faida ya mabao mawili kwa Simba inawapa nafasi ya kuwa na uhakika kutinga hatua ya robo fainali.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.