ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa watafanya kazi kubwa kupata matokeo dhidi ya Al Hilal kutokana na ugumu uliopo kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic tayari imeshatia timu nchini Mauritania kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Januri 12 2025.
Katika mchezo wao uliopita Yanga ilivuna pointi tatu dhidi ya TP Mazembe baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe ambapo mabao mawili yalifungwa na mshambuliaji Clement Mzize.
Kamwe amesema kuwa wanatambua umuhimu wa pointi tatu kwenye mchezo huo hasa ukizingatia wao wana pointi nne na wanahitaji kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali.
“Tunatambua ni mchezo mgumu na tunakwenda kwa tahadhari kwa ajili ya kupata pointi tatu, mashabiki waendelee kutuombea dua na wachezaji wapo tayari kuona kwamba tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu muhimu.”
Kwenye Kundi A, Yanga nafasi ya tatu na pointi 4 huku MC Alger nafasi ya pili na pointi 8 vinara ni Al Hilal wakiwa na pointi 10 na TP Mazembe mwendo wameumaliza kwa kupoteza mchezo wao dhidi ya MC Alger Januari 10 2025.
Katika mchezo huo MC Alger walipata bao la penalti yenye utata likifungwa na Akram Bouras dakika ya 36 kipindi cha kwanza likadumu mpaka dakika ya 90.
Mazembe wanaumaliza mwendo wakiwa na pointi mbili walizopata kwenye mechi tano msimu wa 2024/25 hawajawa kwenye mwendo bora na mchezo mmoja mkononi hata wakishinda hawatapenya nafasi yoyote.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.