KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Kibu Dennis amesema kuwa malego makubwa ni kuona wanapata matokeo katika mechi za kitaifa na kimataifa ndani ya uwanja kutokana na ushirikiano uliopo.
Kibu ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ambapo kwenye mechi 15 za ligi ni 11 alipata nafasi ya kucheza akikosekana kwenye mechi 4 pekee.
Simba ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 40 kibindoni safu ya ushambuliaji imefunga mabao 31 na Yanga ni namba mbili kwenye msimamo pointi 39 huku safu ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 32.
Nyota huyo ameweka wazi kuwa ushindani ni mkubwa ndani ya ligi hilo wanalitambua hivyo wanapambana kufanya vizuri katika mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja.
“Ushindani ni mkubwa ndani ya uwanja kutokana na kila timu kuwa tayari kutafuta ushindi ipo hivyo kama ambavyo ilikuwa kwenye mchezo dhidi yaSingida Black Stars na mechi nyingine lakini malengo yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri.”
Simba kete yao ijayo kimataifa inatarajiwa kuchezwa nchini Tunisia itakuwa ni Januari 5 dhidi ya SC Sfaxine ambapo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 2-1 mabao yote ya Simba yakifungwa na Kibu Dennis.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.