WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KUAGA MWILI WA MAREHEMU JAJI WEREMA
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 02, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuaga mwili wa marehemu Jaji Fredrick Werema ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2009-2014. Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amesikitishwa na kifo cha Jaji Werema na amemtaja kama kiongozi shupavu…