BITTECH YAWASHIKA MKONO WATOTO YATIMA MAGOMENI, DAR

Kampuni ya Bittech kwa kushirikiana na KMC FC imefanya zoezi la kugawa vifaa vya shule kwa watoto yatima wa Umra. Zoezi hilo la utoaji ilifanyika katika kituo cha watoto yatima cha Umra kilichopo Magomeni Mikumi, ambapo watoto wengi walifaidika na msaada huo muhimu.

Akizungumza katika zoezi hilo la utoaji wa vifaa vya shule, Mhariri wa Kampuni ya Bittech, Bi Nancy Ingram amesema kuwa, “Tuna furaha kubwa kushirikiana na KMC FC katika kuunga mkono jamii yetu, hasa watoto yatima ambao mara nyingi wanakosa fursa muhimu kama vile vifaa vya shule. Kampuni yetu ina dhamira ya kutoa msaada kwa watoto hawa ili waweze kupata elimu bora na kufikia malengo yao.”

Ukiachana na hilo kumbuka pia kubashiri na Meridianbet ambapo odds kubwa na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Aliendelea kusema kuwa “Watoto hawa ndio viongozi wa baadae, na elimu ndio ya msingi kwa mtoto, vifaa hivi vikasaidie watoto hawa ili wakasome vizuri bila kuwaza kupungukiwa na vitu vya shule”.

Baada ya kupokea vifaa hivyo wenyeji wa eneo hilo walitoa neno lao la shukrani sana na kusema kuwa ujio huo wa Bittech umekuwa kama mwanga kwao kwani ni watu wachache sana ambao wanajitoa kusaidia wengine wenye uhitaji hivyo wanashukuru sana.

Vifaa vilivyogawiwa vilijumuisha madaftari, kalamu, mabegi ya shule, na vifaa vingine vya kimsingi vya shule. Watoto walionekana kuwa na furaha na shukrani kwa msaada waliopokea, huku wakisema kuwa msaada huo utawasaidia kuwa na moyo wa kujituma katika masomo yao.

Kampuni ya Bittech na KMC FC wametangaza kuendelea na juhudi hizi za kusaidia watoto katika jamii na kuhamasisha wadau wengine kuungana nao katika shughuli za kijamii ambazo zinalenga kuboresha maisha ya watoto na vijana.

Hii ni hatua nyingine muhimu katika kukuza ushirikiano wa kijamii na kukuza maendeleo ya elimu nchini, ambapo Bittech na KMC FC wameonyesha kujitolea kwa dhati kwa ustawi wa watoto yatima na jamii kwa ujumla.