GUSA ACHIA TWENDE KWAO YA YANGA YAIPIGA MKONO FOUNTAIN GATE

GUSA achia twende kwao ya Yanga leo Desemba 29, 2024 imezaa jumla ya magoli 13 kwenye mechi tatu zilizopita baada ya kushusha kipigo cha 5-0 dhidi ya Fountain Gate Fc katika dimba la KMC Complex.

Yanga ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi imefunga jumla ya magoli 32 huku ikiruhusu magoli sita na kukusanya pointi 39 baada ya mechi 15 za mzunguko wa kwanza.

Yanga Sc 5-0 Fountain Gate
16’ Pacome
45+1’ Pacome
41’ Mudathir
51’ Jackson (OG)
87’ Mzize