MASTAA wanne Yanga bado hali zao hazijawa imara kutokana na kutokuwa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mechi zao za ushindani zilizopita hivyo kuna hatihati wakakosekana kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mashujaa, Uwanja wa KMC, Complex.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo wachezaji ambao bado hawajawa imara kwa ajili ya mechi zao zijazo huku taarifa kutoka kwenye jopo la madaktari itaamua kuhusu kucheza kwao kwenye mechi zijazo.
Ni Clatous Chama ambaye ni kiungo, Djigui Diarra ambaye ni kipa, Chadrack Boka, Aziz Andambwile hawa huenda watakosekana kwenye mechi zijazo za ushindani ndani ya kikosi cha Yanga.
Kamwe amesema: “Clatous Chama alipata maumivu ya mkono kwenye mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe sehemu yake ya kiwiko hali yake haikuwa nzuri baada ya kufanyiwa vipimo ameonekana kwamba hajavunjika
“Boka ni nusunusu kurejea kwenye ubora wake tunasubiri taarifa kutoka kwenye kitengo cha utimamu wa mwili ili kutupa ruhusa ya kuendelea kuwatumia, Aziz Andambwile bado hajarejea kwenye ubora wake.
“Hali ya mlinda mlango wetu namba moja Djigui Diarra ambaye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe bahati mbaya alikuwa na shida kwenye nyama za paja hivyo tulidhani pengine ni tatizo hilo lakini baada ya vipimo iligundulika ni sehemu ya kigimbi na sio shida sana.
“Baada ya dakika 45 za kwanza alishindwa kuendelea na mchezo akaingia Khomein Aboubhakr, baada ya vipimo ilibainika kwamba alipata maumivu kwenye gimbi lake hivyo tunasubiri ripoti ya daktari kama ataweza kucheza mechi zijazo ikiwa itakuwa tofauti basi tutajua nani ataanza kwenye mchezo wetu ujao.
“Yupo Aboutwalib Mshery, Khomein hawa wote ni makipa wazuri hatuna mashaka nao tuna amini watafanya kazi kubwa ikiwa watapata nasi kwenye mechi zetu.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.