SIMBA KUBADILI MBINU MBELE YA KEN GOLD

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema kuwa kuelekea katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ken Gold watabadili mbinu kupata matokeo chanya.

Simba itawakaribisha Ken Gold, Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa kwaza unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Timu hiyo metoka kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya SC Sxfaxine uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo ilikomba pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-1 na mabao yote ya Simba yalifungwa na Kibu Dennis dakika ya 7 na dakika ya 90.

Fadlu amesema wanatambua ushindani ni mkubwa ndani ya uwanja kutokana na kila timu kuhitaji pointi tatu hivyo wataingia kwa tahadhari kwenye mchezo huo kutafuta pointi tatu muhimu.

“Ni mchezo muhimu kwetu na utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu inahiji pointi tatu, tupo tayari na ninawapongeza wachezaji kutokana na mwendelezo mzuri katika mechi zetu ambazo zimepita hivyo tunaamini makosa tunayafanyia kazi kuwa bora.

 “Tumekuwa na mwendo mzuri katika mechi zetu ambazo zimepita na kuelekea katika mchezo ujao tutabadili mbinu kupata matokeo, mashabiki wamekuwa nasi tunapenda kuona wakiendelea kuja kwenye mechi zetu kwani wanaongeza nguvu kwa wachezaji kupambana kila wakati.”

Simba kwenye msimamo ni nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 11 ikiwa na pointi 28 kibindoni Ken Gold ni nafasi ya 16 ikiwa na pointi 6 baada ya kucheza mechi 14.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.