MUTALE AWEKWA BENCHI, AHOUA NAYE

KIUNGO Joshua Mutale ameanza benchi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ken Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Wengine waliopo benchi ni Ally Salim, Hamza, Zimbwe Jr, Kagoma, Okejapha, Jean Ahoua, Mukwala, Mashaka na Alexander.

Kikosi cha kwanza ni Camara, Kijili, Nouma, Chamou, Che Malone, Mzamiru Yassin akiwa na kitambaa cha unahodha.

Ladack Chasambi, Fabrice Ngoma, Leonel Ateba, Awesu Awesu na Kibu D mkandaji. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita wa kimataifa Kombe la Shirikisho Afrika, Kibu alifunga mabao mawili wakivuna pointi tatu Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.