VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam FC leo watakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Fountain Gate mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ipo wazi kwamba namba moja kwenye ligi ni Azam FC ikiwa na pointi 30 baada ya mechi 14 inakutana na Fountain Gate iliyo nafasi ya 6 na pointi 20.
Tabora United yenye pointi 24 ambayo imetoka kuvuna pointi tatu mbele ya Azam FC itakuwa uwanjani saa 8 mchana kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union iliyo nafasi ya 10 na pointi 16.
Desemba 18 2024 itakuwa ni Simba yenye pointi 28 nafasi ya tatu v Ken Gold yenye pointi 6 nafasi ya 16 Uwanja wa KMC Complex saa 10:00.
Desemba 16 2024 NBC Premier League iliendelea na matokeo ilikuwa namna hii:-
Tanzania Prisons 0-2 Singida Black Stars kwa mabao ya Marouf Tchakei dakika ya 48 na Kennedy Juma dakika ya 62, Uwanja wa Sokoine.
KMC 1-0 Pamba Jiji kwa bao la Hance Masoud dakika ya 88 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Singida Black Stars ni namba mbili kwenye msimamo ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 14.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.