MNYAMA Simba kwenye anga la kimataifa amefanya yake kwa kukomba pointi tatu mbele ya wapinzani wao Waarabu kutoka Tunisia kwa kupata ushindi jioni katika dakika za lala salama.
Baada ya dakika 90 ubao umesoma Simba SC 2-1 CS Sfaxien ambapo hawa walianza kufunga bao mapema dakika ya 3 kupitia kwa Hazem Hassen akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Simba inayoongozwa na Che Malone.
Kibu Dennis mkandaji aliibuka nyota wa mchezo kwa kufunga mabao yote mawili kwa mapigo ya vichwa alianza dakika ya 7 akitumia pasi ya Jean Ahoua ambaye alikwama kusepa na dakika 90 kwenye mchezo wa leo.
Bao la pili Kibu kafunga dakika ya 90 ikiwa ni muda anaosubiriwa mwamuzi kukamilisha mchezo na wapinzani wakiamini kwamba wanasepa na pointi moja Uwanja wa Mkapa.
Simba inakusanya pointi sita baada ya kucheza mechi tatu katika Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya makundi nafasi ya pili.
Bao la Kibu limezua balaa baada ya benchi la ufundi la SC Sfaxine kuonekana likilalamika kuhusu muda na kumzonga mwamuzi baada ya mchezo kukamilika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.