WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika, Simba ikiwa ni hatua ya makundi watakuwa kazini Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu.
Ni mchezo muhimu dhidi ya SC Sfaxien ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki ambao wamejitokeza kwa wingi uwanjani.
Hiki hapa kikosi kinachotarajiwa kuanza:- Mousa Camara, Fabrice Ngoma, Jean Ahoua, Shomari Kapombe, Leonel Ateba, Hamza, Zimbwe Jr, Mavambo, Che Malone, Awesu Awesu, Kibu Dennis.
Kiungo mkabaji Awesu Awesu ameanza kikosi cha kwanza kwenye anga la kimataifa dhidi ya SC Sfaxine hivyo ana kazi kubwa kumuonesha kocha Fadlu Davids kwamba hajakosea kumpa nafasi hiyo katika anga la kimataifa.
Wachezaji wa akiba ni Aishi Manula, Chamou, Nouma, Mzamiru Yassin, Okejapha, Mutale, Chasambi na Mukwala, Yusuph Kagoma.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.