KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum ni namba moja katika wakali wa kutengeneza pasi za mwisho ndani ya NBC Premier League msimu wa 2024/25.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/34 nyota huyo alitoa jumla ya pasi saba alikuwa ni namba mbili na namba moja alikuwa Aziz Ki wa Yanga aliyetoa pasi 8.
Ki kwa sasa ni pasi mbili za mabao ametoa akiwa na uzi wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic, mashine ya Ujerumani.
Rekodi zinaonyesha kuwa pasi ya kwanza kwa Fei Toto alitoa kwenye mchezo dhidi ya KMC, uliochezwa Uwanja wa KMC Complex mzunguko wa kwanza ilikuwa ni Septemba 19 2024.
Katika mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora kutokana na kuonyesha kiwango bora na kutengeneza pasi mbili za mabao.
Pasi ya kwanza alimpa Idd Suleiman Nado ilikuwa dakika 19 na pasi ya pili alimpa Lusajo Mwaikenda ilikuwa dakika 54.
Pasi ya tatu alimpa Nassoro Saadun dakika ya 9 ilikuwa dhidi ya Coastal Union ya Tanga mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Septemba 22 2024.
Pasi ya nne alimpa Lusajo ilikuwa dhidi ya Namungo Oktoba 3 2024 Uwanja wa Majaliwa dakika ya 76. Pasi ya tano alimpa Saadun dakika ya 10 kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Desemba Mosi 2024.
Data hizi ni kwa mujibu wa Azam TV kupitia mechi zake zinazorushwa mubashara, kuwa katika mechi husika siku ya mechi za NBC Premier League.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.