KIKOSI cha Yanga kimewasili salama nchini DR Congo baada ya kukwea pipa Desemba 12 2024 ikiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 14 2024 utakuwa ni watatu kwa Yanga kushuka uwanjani katika anga la kimataifa.
Kwenye orodha hiyo kuna makipa watatu, viungo 12, washambuliaji watatu na mabeki 7 hivyo ni msafara wa wachezaji 25 chini ya Kocha Mkuu Sead Ramovic.
Hii hapa orodha yao:-Makipa
Diarra, Khomein, Mshery.
Mabeki
Nondo, Job, Bacca, Yao, Kibabage, Kibwana na Boka.
Viungo
Aucho, Mudathir, Mkude, Abuya, Maxi, Nkane, Sure Boy, Farid, Sheikhan, Pacome, Chama, Aziz.
Washambuliaji
Musonda, Mzize na Dube.